1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Wakuu wa Soudan na SPLM wafikia makubaliano ya kugawana mali asili ya nchi yao

6 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlg
Wakuu wa Sudan na viongozi wa chama cha waasi SPLM, wamesema wamefikia makubaliano ya kugawana mali asili ya nchi yao, katika majadiliano ya kumaliza vita vya zaidi ya miaka ishirini, yanayofanyika katika mji wa Naivasha, karibu na mji mkuu wa Kenya- Nairobi.
Msemaji wa chama cha SPLM Bwana Yasser Arman, amewaambia waandishi wa habari, kwamba swali la kugawana mali asili ya Sudan lilikua miongoni mwa maswali tete yaliyochelewesha mazungumzo, akasema mkataba wa makubaliano kuhusu kugawana utajiri wa nchi yao wakati wa kipindi cha uongozi wa mpito, utasainiwa kesho ijumatano.
Soudan ina utajiri wa mafuta ya petroli, na kulingana na takwimu zilizopo wakati huu, nchi hiyo ina uwezo wa kuzalisha mapipa zaidi ya laki tatu kwa siku.