1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Waasi wa LRA wamuua raia wa Uingereza

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKo

Watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi la Lord´s Resistance Army la Uganda wamempiga risasi na kumuua mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada, kusini mwa Sudan. Collin Lee, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 67 na mkewe mjamzito walikuwa wakisafiri kutoka Uganda kuelekea mji wa Yei nchini Sudan wakati waliposhambuliwa yapata kilomita 12 kutoka mpakani.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la International Aid Services kusini mwa Sudan, Onesimo Yugusuk, amethibitisha kwamba Collin alipigwa risasi kifuani na kufariki dunia siku ya Jumamosi. Mkewe hakujeruhiwa lakini dereva wao alipigwa risasi mkononi na anaendelea kupata matibabu hosptalini mjini Kampala.