NAIROBI: Viongozi kujadili njia za kulinda hali ya hewa
15 Novemba 2006Matangazo
Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani unaofanywa mji mkuu wa Kenya Nairobi unaingia katika awamu muhimu leo hii. Mawaziri wa mazingira wa nchi 189 zinazoshiriki katika mkutano huo au wajumbe wao watashauriana kwa siku tatu.Mada kuu ni mustakabali wa itifaki ya kuhifadhi hali ya hewa na utaratibu wa kuzisaidia nchi zinazoendelea.