Nairobi. Tume ya haki za binadamu yaonyesha ushahidi mwingine wa mauaji.
7 Novemba 2007Wakionyesha ripoti za uchunguzi wa maiti kwa baadhi ya watu karibu 500 wanaosemekana wameuwawa na maafisa wa polisi, kundi la kutetea haki za binadamu nchini Kenya limepinga ukosoaji wa jeshi la polisi na kurudia wito wao wa kufanyika kwa uchuguzi wa kimataifa.
Polisi wa Kenya wamekana kufanya mauaji yoyote, ambayo yalifanyika wakati wa msako dhidi ya kundi wa kihalifu la Mungiki mapema mwaka huu.
Siku ya Jumanne polisi waliyaeleza madai kuwa maafisa wa jeshi hilo wamehusika na mauaji hayo kuwa ni ya kijeuri na dharau.
Tume ya haki za binadamu nchini Kenya leo imewaonyesha waandishi wa habari nakala za ripoti za uchunguzi wa maiti za vijana kadha ambao walihusika katika msako, ambapo wote walifariki kutokana na kupigwa risasi.