1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Tetemeko la ardhi laikumba Afrika Mashariki

20 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXW

Tetemeko kubwa la ardhi limelikumba eneo la Afrika Mashariki leo. Hayo ni kwa mujibu wa taasisi ya jiolojia ya Marekani, USGS.

Tetemeko hilo ni la pili kufuatia tetemeko lengine lililotokea juzi Jumamosi. Taasisi ya USGS imesema kwenye tovuti yake kwamba tetemeko la kiwango cha 5.2 katika kipimo cha Richter limelitikisa eneo la kaskazini mwa Tanzania, yatapa kilomita 85 kaskazini magharibi mwa mji wa Arusha.

Mitetemeko hiyo imefika hadi mji mkuu wa Kenya, Nairobi, umbali wa kilomita 180, ambako majumba ya makaazi na majengo marefu yalitisikia kidogo kwa dakika kadhaa.

Kenya na Tanzania ziko katika eneo linalokabiliwa na hatari ya mitetemeko la bonde la ufa.

Mitetemeko ya sasa imezusha wasiwasi mpya tangu wafanyakazi kwenye majumba marefu mjini Nairobi walipokimbia kutoka ofisini mwao wakati mji huo ulipokumbwa na mitetemeko kwa siku tano mwezi uliopita.

Maafisa wa jiolojia nchini Kenya hawajathibitisha kitovu cha mitetemeko ya mwishoni mwa juma.