Nairobi. Mkutano wa hali ya hewa wataka kupitiwa upya kwa makubaliano ya Kyoto.
19 Novemba 2006Mkutano wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa umemalizika katika mji mkuu wa Kenya , Nairobi, kwa makubaliano ya kupitia upya vipengee vya mkataba wa Kyoto mwaka 2008.
Mkataba wa Kyoto unatarajiwa kumalizika muda wake mwaka 2012.
Makundi ya harakati za ulinzi wa mazingira kama Greenpiece na marafiki wa Dunia , Friends of the Earth pamoja na baadhi ya wajumbe wa Afrika katika mkutano huo wameeleza masikitiko yao kuwa hakuna kilichopatikana kikubwa katika mazungumzo hayo ya wiki mbili. Mawaziri wa mazingira waliohudhuria mkutano huo , ikiwa ni pamoja na waziri wa Ujerumani Sigmar Gabriel pia wamekubali kuyashawishi mataifa tajiri kusaidia upunguzaji wa gesi zinazochafua mazingira barani Afrika. Katika taarifa , umoja wa Ulaya umesifu kile ilichokiita hatua madhubuti zilizopigwa katika mkutano huo wa Nairobi.