1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mabadiliko ya hali ya hewa yahatarisha amani na usalama duniani

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema,mabadiliko ya hali ya hewa yanahatarisha amani na usalama duniani.Alipohotubia mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Nairobi,Kenya,Annan alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kulipa umuhimu suala la mabadiliko ya hali ya hewa sawa na hatua zinazochukuliwa kuzuia vita,kuzuia silaha za maangamizi na kupambana na umasikini.Mkutano huo ulifikia kilele siku ya Jumatano baada ya mawaziri wa mazingira kuwasili Nairobi kuendelea na majadiliano hadi siku ya Ijumaa.Wajumbe mkutanoni wamekubali kuwa na fuko la fedha kuzisaidia nchi masikini kukabiliana na ujoto duniani.