1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Kenya yawarejesha kwao wakimbizi wa Ethiopia

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPv

Serikali ya Kenya imewarudisha kwao Waethiopia takriban 1,000 waliokimbia nchi yao kufuatia machafuko yaliyozuka nchini humo hivi majuzi.

Waethiopia hao wa makabila ya Gabra na Borana, ambao wamekuwa wakipigania mifugo, maeneo ya malisho na maji, walirudishwa baada ya serikali ya Ethiopia kuwahakikishia usalama nchini mwao.

Watu hao walivuka mpaka na kuingia Kenya siku nne zilizopita na kundi hilo lililokuwa na idadi kubwa ya wanawake na watoto, lilikuwa likiishi karibu na mji wa mpakani wa Moyale nchini Kenya.

Imeripotiwa kwamba polisi walitumia nguvu kuwatimua Waethiopia hao.