1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Ethiopia yadaiwa maelezo juu ya mahabusu

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCD

Ethiopia imekuwa kwenye shinikizo hapo jana la kuitaka itowe maelezo ya mahabusu kutoka nchi 19 wanaoshikiliwa katika magereza ya siri nchini humo ambao mashushu wa Marekani wamekuwa wakiendesha usaili katika msako wa Al Qaida katika eneo la Pembe ya Afrika.

Canada,Sweden na Eritrea zimekuwa zikishinikiza kutolewa kwa habari juu raia wao walioko nchini Etihiopia ambapo makundi ya haki za binaadamu yanasema mamia ya wafungwa wakiwemo wanawake na watoto wamekuwa wakihamishiwa nchini humo kwa siri na kinyume na sheria.

Uchunguzi wa shirika la habari la Associated Press umegunduwa kwamba mashushu wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA pamoja na Shirika la Upelelezi la FBI wamekuwa wakiwasaili mahabusu hao.

Baadhi ya mahabusu hao wamesombwa na wanajeshi wa Ethiopia wakati walipoitimua serikali ya itikadi kali ya Kiislam nchini Somalia mwishoni mwa mwaka jana na wengine wamekuwa wakisafirishwa kutoka Kenya ambapo Wasomali wengi wamekuwa wakiendelea kukimbia umwagaji damu nchini mwao.