1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Ethiopia na Eritrea yumkini kurudia vitani

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79o

Mahasimu wa Pembe ya Afrika Ethiopia na Eritrea yumkini zikarudia tena vitani kuhusu mzozo wao wa mpaka katika kipindi cha wiki chache iwapo hakutokuwepo kwa msukumo mkubwa wa kimataifa kuwazuwiya.

Vita vya mwaka 1998 hadi 2000 kwenye mpaka viliuwa watu 70,000 na kupelekea dhiki kubwa kwa watu wa nchi hizo maskini kabisa duniani.

Hivi sasa wachambuzi wa mambo wanaonya juu ya kurudia kulimbikizwa kwa wanajeshi mipakani kabla ya tarehe ya mwisho mwishoni mwa mwezi wa Novemba iliowekwa na tume huru ya mipaka kwa Ethiopia na Eritrea kuchora mipaka yao.