NAIROBI : Eritrea yadai Ethiopia yajiandaa kwa vita
3 Novemba 2007Matangazo
Eritrea leo imeituhumu hasimu wake mkuu Ethiopia kwa kujiandaa kuanzisha vita vyengine na kuzidisha hali ya wasi wasi kwamba nchi hizo jirani za Pembe ya Afrika yumkini zikarudia kupigana juu ya mzozo wa mipaka.
Gazeti la serikali ya Eritrea limesema habari hizo zimetolewa na wananjeshi watatu wa Ethiopia waliokimbia jeshini na kuvuka mpaka wa hatari ambapo inarepotiwa kuwa walinzi wa mpakani huuwa kwa kuwapiga risasi mtu yoyote yule anayethubutu kuvuka mpaka.
Hali ya mvutano imekuwa ikiongezeka baina ya nchi hizo ambazo zimekuwa kwenye uhasama tokea mzozo wao wa umwagaji damu wa mwaka 1998-2000 ambapo kwayo watu 70,000 waliuwawa.