1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu Kansela wa Ujerumani ziarani Ukraine

3 Aprili 2023

Naibu Kansela wa Ujerumani Robert Habeck amewasili nchini Ukraine katika ziara ya ghafla ambayo anaifanya kwa mara ya kwanza tangu vita vilipozuka katika nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4PcrN
Vizekanzler Habeck in der Ukraine
Picha: Christoph Soeder/picture alliance/dpa

Kwa mujibu wa gazeti la the Spiegel la Ujerumani, Habeck ambaye pia ni waziri wa nishati na uchumi  atajadili kuhusu suala la ujenzi mpya wa Ukraine pamoja na ushirikiano katika sekta ya nishati.

Ziara ya Habeck imethibitishwa pia na msemaji wa wizara yake ingawa hakutowa maelezo zaidi kutokana na tahadhari za kiusalama.

Sekta ya nishati ya Ukraine imeshambuliwa mara kadhaa na Urusi katika vita vinavyoendelea na baadhi ya wakati mamilioni ya watu waliachwa kizani kutokana na kuharibiwa kwa miundo mbinu ya umeme.