NAGASAKI: Japan yakumbuka shambulio la bomu la atomu
9 Agosti 2006Matangazo
Japan imeadhimisha mwaka wa 61 tangu bomu la pili la atomu kudondoshwa katika mji wa Nagasaki. Waziri mkuu wa Japan,Junichiro Koizumi amehudhuria kumbukumbu ya shambulio hilo la bomu lililoua watu wapatao 74,000 na kuwajeruhi zaidi ya 40,000 wengine.Meya wa Nagasaki,Itscho Ito ameikosoa miradi ya kinuklia ya Iran na Korea ya Kaskazini.Vile vile ameituhumu Marekani kuwa haichukuwi hatua imara kupunguza mrundiko wa silaha zake za kinuklia.Siku ya Jumapili,mji wa Hiroshima uliadhimisha kumbukumbu ya shambulio la kwanza la bomu la atomu lililofanywa duniani.