Na hatimaye soka: AC Milan yaibuka kidedea.
5 Mei 2005Matangazo
AC Milan imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya , Champions League licha ya kufungwa mabao 3-1 dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi katika pambano lao la nusu fainali mchezo wa pili jana. Timu hiyo kutoka Milan nchini Itali imenusurika kutokana na sheria ya goli la ugenini kutokana na timu hizo kumaliza michezo yao miwili ikiwa sare kwa kufungana jumla ya mabao 3-3. AC Milan sasa itakumbana na FC Liverpool ya Uingereza katika fainali mjini Istanbul hapo May 25.