Na hatimaye michezo: Mpiga mbio wa Ethiopia avunja rekodi.
27 Agosti 2005Matangazo
Katika riadha Muethiopia Kenenisa Bekele ameivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 10,000 wanaume.
Mpiga mbio huyo wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 23 alitumia dakika 26 na sekunde 17.53 katika mashindano ya Golden League mjini Brussels jana na kuvunja rekodi yake ya zamani ya dakika 26 : 20.31 aliyoiweka Juni huko Ostrava , 2004.