MZOZO WA ZIMBABWE WATAWALA MKUTANO:
6 Desemba 2003Matangazo
ABUJA: Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola-Commonwealth umefunguliwa katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.Mkutano huo wa madola 52 ukiwakilisha theluthi moja ya umma duniani umefunguliwa rasmi Ijumaa na Malkia Elizabeth wa Uingereza.Mwenyeji Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria,katika hotuba yake ya ufunguzi,amesema Jumuiya ya Madola yapaswa kukabiliana na matatizo ya karne ya 21.Kwa upande mwingine mabishano kuhusika na kutoalikwa Zimbabwe yalichukua sehemu kubwa ya majadiliano ya siku ya mwanzo.Madola ya Kiafrika yametoa wito wa kuiruhusu Zimbabwe kurejea kwenye jumuiya hiyo,wakati nchi za magharibi zinaunga mkono hatua ya kuendelea kuizuia Zimbabwe kuhusika na mzozo kuwa Rais Robert Mugabe alifanya udanganyifu wakati wa uchaguzi uliomrejesha madarakani.Na Rais Mugabe amelituhumu kundi hilo kuwa linaingilia mamlaka ya nchi yake.Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema ni vitendo vya Mugabe vilivyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuitenga Zimbabwe.Hiyo jana Don McKinnon alichaguliwa tena kwa kipindi cha pili kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.