Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, hali ya sintofahamu inaripotiwa mjini Uvira katika mkoa wa Kivu kusini ambapo baada ya wakaazi kupinga uteuzi wa kiongozi mmoja wa kabila la Banyamulenge aliyeteuliwa hivi karibuni kuongoza eneo la Bijombo katika wilaya hiyo ya Uvira. Kutoka Bukavu, mwandishi habari wetu Mitima Delachance ametutumia taarifa ifuatayo.