Mzozo kuhusu makombora ya Taurus Ukraine waendelea Ujerumani
12 Machi 2024Matangazo
Wasiwasi ulishuhudiwa ndani ya muungano unaotawala hapo jana wakati mzozo huo kuhusu kupeleka makombora ya Taurus Ukraine ulipoendelea na kuchochewa kuwa mkubwa na hatua hiyo ya Urusi kuchapisha mazungumzo kati ya maafisa wa jeshi la Ujerumani.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amefutilia mbali kupeleka makombora hayo Ukraine angalau kwa sasa, akisema masafa yake ni marefu mno na kwamba Ujerumani huenda ikaburuzwa katika vita vya moja kwa moja iwapo itajaribu kuyapeleka.
Hata hivyo vyama vya upinzani vya Christian Democratic Union CDU na Christian Social Union, CSU, vinaliunga mkono wazo hilo na vinaandaa kura kadhaa bungeni vikipendekeza makombora hayo yapelekwe Ukraine. Kura inayofauta imepangwa kufanyika Alhamisi wiki hii.