Mwito kwa China kupandisha thamani ya sarafu yake
28 Novemba 2007Matangazo
Wanasiasa wa Umoja wa Ulaya wanaokutana na wajumbe wa serikali ya China mjini Beijing wameeleza wasiwasi wao kuhusika na nakisi ya biashara,inayozidi kuwa kubwa kati ya Ulaya na China.
Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso ametoa mwito kwa China kupunguza vikwazo vya biashara na kupandisha thamani ya sarafu yake.Ni matumaini ya Umoja wa Ulaya kuwa masuala ya kiuchumi yataweza kutenzuliwa pamoja na China katika mkutano huo wa kilele mjini Beijing.Umoja wa Ulaya ni soko kubwa kabisa la China,na mwaka huu umoja huo unatathmini kuwa nakisi ya biashara itafikia Euro bilioni 170.