Baada ya viongozi wawili wa siasa kali za kizalendo wa Ulaya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Jumapili, mmoja wa viongozi wa kwanza wa kigeni kuwapongeza wote wawili hakuwa kutoka nchi jirani au mshirika wa kikanda. Alikuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin. Mwangaza wa Ulaya, unaangazia chaguzi mbili zilizofanyika Ulaya na kuwapa ushindi mkubwa wanasiasa wenye misimamo mikali ya kizalendo.