Japokuwa gari ni chombo muhimu katika kumrahisishia mwanaadamu usafiri na shughuli zake za kimaisha, lakini pia ni miongoni mwa vyanzo vikubwa kabisa vya uchafuzi wa mazingira, ambao hupelekea athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi zinazowaumiza maelfu ya watu duniani hivi sasa. Ndio maana mji wa Pontevedra nchini Uhispania umeamua kupiga marufuku magari yasiyo ya lazima kuingia mjini humo.