Ufaransa imekuwa ikikabiliwa katika siku za hivi karibuni na maandamano makubwa kutokana na raia wa nchi hiyo kupinga vikali mpango wa mageuzi ya pensheni ambayo yatapelekea miongoni mwa mambo mengine, umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64. Lakini Je, mifumo ya pensheni katika mataifa mengine ya Ulaya inaweza kulinganishwa na ile ya Ufaransa?