1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha Kipyegon Bett afariki dunia akiwa na miaka 26

7 Oktoba 2024

Mshindi wa zamani wa dunia wa medali ya shaba kwenye mbio za mita 800 Kipyegon Bett amefariki jana Jumapili akiwa na umri wa miaka 26 baada ya figo na ini kushindwa kufanya kazi.

https://p.dw.com/p/4lVK2
Mmoja ya wanariadha wa nchini Kenya katika mbio za kimataifa
Matumizi ya dawa za kusisimua misuli zimeitia doa tasnia ya riadha nchini KenyaPicha: Reuters//D. Ebenbichler

Raia huyo wa Kenya alikuwa mmoja wa wanariadha waliokuwa na matumaini makubwa lakini mnamo mwaka 2018 kitengo kinachosimamia uadilifu wa wanariadha duniani (AIU) kilimpiga marufuku kushiriki kwenye michuano kwa miaka minne baada ya kukutwa na chembechembe za dawa za kuongeza nguvu mwilini mwake.

Bett alikanusha kuwahi kutumia dawa hizo za kuongeza kasi ya mzunguuko wa damu.

Kashfa nyingi za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini zimeharibu sifa ya Kenya kama kinara wa riadha. Katika kipindi cha miaka mitatu pekee iliyopita, takriban wanariadha 80 kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki wamewekewa vikwazo.