Mwanajeshi wa Kijerumani awauwa watu wanne kwa risasi
1 Machi 2024Matangazo
Miongoni mwa waliouawa kwenye mashambulizi hayo ni mtoto mdogo.
Wachunguzi hawakutoa maelezo zaidi kuhusu waathirika wa tukio hilo, kama vile umri, jinsia au uhusiano wao na mshukiwa.
Mshukiwa wa uhalifu huo alijisalimisha baada ya shambulizi hilo na kukamatwa, wachunguzi walisema.
Polisi walisema mivutano ya ndani ya nyumba inaweza kuwa sehemu ya uchunguzi wao kwenye chanzo cha uhalifu huo.