1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanachama wa PLO afariki

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSkx

Afisa wa cheo cha juu wa chama cha Palestine Liberation Organisation, PLO, Emile Jarjoui, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kufuatia mshutuko wa moyo.

Familia yake imesema leo Jarjoui aliyekuwa na umri wa miaka 72, amefariki nyumbani kwake mjini Bethlehem. Alikuwa mwanachama wa kamati tekelezi ya chama cha PLO aliyeyashughulikia maswala ya wakristo katika mamlaka ya Waplestina.

Kufariki kwa Emile Jarjoui kunawaacha wanachama 12 wa PLO. Watano kati ya wanachama 18 wa kamati hiyo walikufa vifo vya kawaida na mmoja akajiuzulu baada ya uchaguzi kufanywa mnamo mwaka wa 1996.

Maafisa wanasita kukifanyia mageuzi chama cha PLO ambayo yatakiruhusu chama cha Hamas, hasimu mkubwa wa chama cha Fatah, kijiunge.

Wakati haya yakiarifiwa Israel imekabiliwa na tetemeko dogo la ardhi mapema leo la kiwango cha 4.2 kwenye kipimo cha Richter. Tetemeko hilo halikusababisha uharibifu wala majeruhi.