1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwakilishsi wa juu wa Waislam azuru Auschwitz

Oumilkheir Hamidou
22 Januari 2020

Hadi wakati huu ni waumini wachache wa Kiislam waliowahi kutembelea kambi za maangamizi ya Wayahudi za Auschwistz-Birkenau. Hivi sasa mwakilishi wa juu wa Waislam na wenzao wayahudi wanazuru kwa pamoja kambi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/3WcmY
70th anniversary of Auschwitz liberation by Red Army
Picha: picture alliance/dpa

Raed Saleh amepata fursa ya kuwaongoza wanafunzi wa kiislam kuitembelea kambi ya mateso na maangamizi ya wayahudi ya Auschwitz."Akizungumza na DW Raed Saleh ambae ni mwenyekiti wa kundi la wabunge wa chama cha Social Democrat katika bunge  la jimbo la Berlin anasimulia jinsi yeye na kundi kubwa  la wanafunzi  walivyokuwa walipoitembelea kwa mara ya kwanza kambi nambari tano za maangamizi na mateso za Auschwitz-Birkenau mnamo mwaka 2013. Katika kambi hizo zilizoko nchini Poland wanazi waliwauwa watu zaidi ya milioni moja na laki moja, vita vikuu vya pili vya dunia vuilipokuwa vikiendelea hadi mwaka 1945.

Raed alifuatana na vijana wa kutoka mazingira na dini tofauti na ambao kawaida hisia za chuki dhidi ya wayahudi si jambo geni . Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 42 binafsi alizaliwa Sebaste kaskazini mwa ukingo wa magharibi kabla ya kuhamia Ujerumani akiwa na umri wa miaka 5. Uamuzi wake wa kwenda Auschwitz umewasisimua wengi nchini Ujerumani. Hadi wakati huu alikuwa muumini wa kwanza wa dini ya kiislam kuzuru kambi za maangamizi na mazeso za Auschwitz-Berkenau-kambi ambazo zinaangaliwa kama ushahiidi wa jinsi wayahudi walivyoteseka katika mauwaji ya halaiki ya Holocaust.

Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia waaizuru kwa pamoja tarehe 2.05.2019 kambi za mateso na maangamizi za Auschwitz-Birkenau
Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia walizuru kwa pamoja tarehe 2.05.2019 kambi za mateso na maangamizi za Auschwitz-BirkenauPicha: picture alliance/dpa/ZUMA/D. Klamka

Mamilioni ya watu wanazitembelea kambi za maangamizi za Auschwitz kila mwaka

 Mwaka 2019 zaidi ya watu milioni mbili na laki tatu waliizuru kambi za maangamizi za Auschwitz-Birkenau. Mkurugenzi wa kambi hizo Piotr Cywinski aliiambia DW "wachache tu walikuwa wa kutoka nchi za kiarabu .Kwa mujibu wa madaftari idadi yao haikupindukia watu 3200. Hata hivyo maafisa wa kituo hicho hawawaulizi watu kuhusu imani yao wanapokuja kuizuru kambi hiyo.Piotr Cywinski anasema katika mahojiano na DW, katika makundi ya watu kutoka Ufaransa, Norway, Ujerumanai na kwengineko kuna watu pia ambao wanaweza kulinganishwa na waislam.

Alkhamisi january 23 kituo hicho kitatembelewa na mwakilishi wa ngazai ya juu kabisa wa dini ya kiislam. Na hilo ni jambo la kusisimua. Mohammed al-Issa ni katibu mkuu wa jumuia ya waislam ulimwenguni, jumuia inayowawakilisha zaidi ya waislam bilioni moja ulimwenguni. Akiwa mwanasiasa wa kutoka Saudi Arabia, aliwahi wakati mmoja kuwa waziri wa sheria pia nchini mwake. Na chanzo cha ziara yake pia kinasisimua. Al Issa atafuatana na mkurugenzi wa baraza la mayahudi wa Marekani AJC-David Harris. Sheikh huyo mwenye umri wa miaka 54, mtaalam wa dini ya kiislam kwa upande mmoja na kwa upande wa pili wakili wa kiyahudi mwenye umri wa miaka 70 ambae binafsi ni mtoto wa manusura wa mauaji ya halaiki ya Holocaust.

Ziara hiyo ya pamoja imesifiwa tangu na wanasiasa mpaka na viongozi wa jumuia za kidini nchini Ujerumani."Hiyo ndio tiba dhidi ya siasa kali za mrengo wa kulia amesema Raed Saleh huku Aiman Matzyek ambae ni mwenyrekiti wa baraza la waislam wa Ujerumani ambae binafsi ameshafuatana mara kadhaa na vijana kzuru kambi za mateso za Auschwitz Birkenau, ameitaja ziara hiyo kuwa ni yenye kuleta matumaini.  Ameitaja Auschwitz kuwa ni funzo kwa waislam pia.

Chanzo: DW