1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano waongezeka kati ya Ulaya na Marekani

28 Oktoba 2013

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi hii leo(28.10.2013) na kashfa inayohusiana na udukuzi wa mawasiliano ya simu uliofanywa na shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA.

https://p.dw.com/p/1A79F
****Die Bilder dürfen ausschließlich zu publizistischen Zwecken im Rahmen des geltenden Presse- und Urheberrechts verwendet werden. Der Abdruck bzw. die Veröffentlichung ist honorarfrei mit dem Vermerk „Foto: Secusmart GmbH".*** Wann wurde das Bild gemacht?: Cebit 2013 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Berlin, Cebit 2013 Bildbeschreibung: Bei welcher Gelegenheit / in welcher Situation wurde das Bild aufgenommen? Wer oder was ist auf dem Bild zu sehen? Angela Merkel bzw. Dr. Hans-Christoph Quelle
Angela Merkel aliyevaa koti jekunduPicha: Secusmart GmbH

Pia wahariri wameandika kuhusu mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na ushindi wa dereva wa mbio za magari ya formula one , Sebastian Vettel, ukiwa ni ushindi kwa Ujerumani.

Gazeti la Berliner Zeitung, linazungumzia kuhusu uhusiano kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani. Gazeti linaandika.

Iwapo mtu atasikiliza mazungumzo kadha yanayofanyika katika bara la Ulaya , pamoja na anayofanya kansela wa Ujerumani, basi hatashangaa kuona ukubwa wa ghadhabu inayoonekana hivi sasa. Zaidi ya hayo ni kwamba vita hii ya siri iliyoanzishwa na shirika la usalama la Marekani inaharibu uhusiano katika ya mataifa ya Ulaya na Marekani, .. ni sumu kali inayozidi kuchochea hisia zinazoharibu hali ya umoja na mshikamano.

Gazeti la Thüringishe Lanseszeitung nalo linazungumzia kuhusu kashfa hiyo. Mhariri anaandika.

Sauti zinapaazwa, kwasababu kwa kweli watu wanahitaji mshikamano na kuaminiana. Kwa kuwa hilo Marekani hailitekelezi , hii ni sawa na kuwa muflisi. Kansela Merkel anapaswa sasa kuchukua hatua , na kuulinda uchumi wa Ujerumani pamoja na wananchi wake. Ujerumani inapaswa kuchukua hatua ya kufanya kuwa vigumu kwa mtu yeyote awe kutoka Marekani ama nchi nyingine yoyote ile kufanya udukuzi nchini humu. Kuzuwia kabisa itakuwa hata hivyo ni vigumu.

Das NSA-Dokument, das zeigt: 2002 begann die Abhöraktion gegen Merkel Quelle: Bild.de Dokument, das der „Spiegel“ zusammen mit anderen NSA-Papieren vom Whistleblower Edward Snowden bekam.
Taarifa zilizodukuliwa na shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA kutoka simu ya mkononi ya kansela Merkel

Gazeti la General Anzeiger la mjini Bonn likizungumzia mada hiyo limeandika.

Marekani inawachukulia washirika wake wa karibu, sio tu Merkel, kama kundi la mifugo yake. Lakini rais Obama hana la kueleza baada ya kutoa maelezo ya juu juu tu kwamba hawajibiki. Iwapo mtu atafuatilia vile rais Obama asivyochukua hatua kuhusu masuala mbali mbali, atatambua kuwa kuna maslahi ya taifa ya kiusalama yanayoikabili dunia hivi sasa na mkakati wa kujaribu kuweka mtazamo mpya.

Marekani haitaki kutambua kuwa hali iliyojitokeza sasa ya udukuzi wa shirika lake la usalama wa taifa itakuwa ndio sababu ya ndoa kuvunjika.

Kuhusu mkutano wa viongozi wa mataifa ya Ulaya, gazeti la Kölner Stadt Anzeiger linaandika.

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya ni mfano wa jinsi Umoja huo unavyoweza kufanyakazi katika siku zijazo. Inahusu hatua ndogo inayoweza kupigwa , na sio kuhusu mpango mkubwa. Bara la Ulaya linayumba yumba kuhusiana na maeneo yake yenye matatizo. Inajengeka taratibu kuhusu sheria zake, na sio kwa mipango mikubwa. Ajenda mpya ya Ulaya ni kuhusu uchumi na utendaji mzuri, lakini hilo si kwa moyo na ubinadamu. Na hilo kwa kweli si kitu kikubwa kuliko msingi wenyewe wa mradi wa Ulaya.

Gazeti la Stuttgart Nachrichten ambalo linazungumzia ushindi wa dereva wa magari ya formula one, Sebastian Vettel, mhariri anasema.

Michael Schumacher alikuwa bingwa wa utendaji usio na makosa, Vettel hatosheki na ushindi. Ni mtu ambaye ataiendesha gari yake kwa kasi kubwa hata katika duru ya mwisho , ili kuhakikisha kuwa anakuwa mtu wa kwanza kuendesha kwa kasi katika duru hiyo. Ni mtu ambaye hatakubali kumzawadia dereva wa timu yake ushindi wa rahisi. Ubinafsi huu umekuwa kwa Schumacher na Vettel msingi wa majadiliano kuhusiana na nani dereva mahiri baina yao, kuwa hauna maana.

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Yusuf , Saumu