mvutano wa mpakani kati ya Ethiopia na Eritrea
12 Oktoba 2007Matangazo
New-York:
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ban Ki-Moon amesema ameingiwa na wasi wasi kutokana na kuzidi makali mzozo kati ya Ethiopia na Eritrea.Wakati huo huo katibu mkuu Ban Kii Boon ameyatolea mwito mataifa hayo jirani yanayohasimiana katika pembe ya Afrika,yajizuwie.Ban Kii Moon amesema hayo ,baada ya rais Girma Wolde-Giorgis wa Ethiopia kuzungumzia azma ya kuzidisha nguvu za jeshi la nchi yake.Ethiopia na Eritrea zinazozana kuhusu eneo la mpaka wa pamoja ambao bado haujachorwa.