Mawakili katika kesi ambayo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inadai fidia kutoka kwa Uganda wamepinga hatua ya Uganda ya kutaka ushahidi wa kuridhisha katika kesi inayosikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya Haki, ICJ kwamba wanajeshi wa Uganda walipora rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya mwaka 1997 na 2003.