Mvutano kati ya rais Trump na wademocrat unaendelea
25 Januari 2019Mpango uliopendekezwa jana na rais Donald Trump na ule mbadala uliopendekezwa na wademokrat ili kuukwamua mzozo wa bajeti haikusaidia kuungwa mkono vya kutosha katika baraza la seneti.
Kwa zaidi ya mwezi sasa wabunge na rais Trump wanazozana kuhusu mada hiyo hiyo: ukuta ambao rais Trump anataka kuujenga katika mpaka wa Marekani na Mexico ili kukabiliana na wahamiaji kinyume na sheria.
Wakiutaja mpango huo kuwa "hauambatani na maadili" na zaidi kuliko yote "hauna maana," wademocrat wanapinga moja kwa moja kutengwa dala bilioni 5.7 ili kuugharimia. Badala yake wanapendekeza hatua nyengine za ulinzi wa mpakani. Matokeo yake tangu decemba 22 iliyopita watumishi laaki nane wa serikali na watumishi wengine kadhaa wanalazimika kusalia majumbani bila ya malipo.
Juhudi za warepublican hazikufaulu
Pendekezo la Republican lililowasilishwa kupigiwa kura kwa mara ya kwanza jana lingesaidia kugharimia shughuli za serikali hadi mwezi wa september na linajumuisha pia fedha za kugharimia ukuta. Repuiblican ndio wanaodhibiti baraza la seneti. Lakini kwa vile wanadhibiti viti 53 kati ya 100, walihitaji kuungwa mkono na wademokrat ili kujipatia sauti 60 zinazohitajika ili pendekezo la rais Trump liweze kufikishwa katika zoezi la mwisho la kupigiwa kura. Hawakufanikiwa kuwatanabahisha wademocrat.
Mara baada ya mapigo yote mawili viongozi wa Republican na Democrat katika baraza la seneti wakakutana kujaribu kuikwamua hali ya mambo.
Ikulu ya Marekani iilidhihirika kuwaachia wasikilizane kuhusu sheria ya kugharimia kwa muda wa wiki tatu kwa masharti kwamba gharama hizo zinajumuisha sehemu kubwa ya fedha za kujenga ukuta.
"Wakiniletea makubaliano ya maana nitayaunga mkono" alisema rais Trump."Bila ya ukuta, hatuwezi kudhamini usalama" amesisitiza mbele ya waandiishi habari.
Trump amebakiwa na karata moja:sheria ya hali ya hatari
Ufumbuzi wowote unabidi upitie katika baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na Democrarts. Na spika wa baraza hilo, Nancy Pelosi ameshasema hakubaliani na akonti ya kugharimia ukuta."
Bado haijulikani kwa hivyo mzozo utafumbuliwa vipi.
Rais Donald Trump anaonyesha kuwa na njia mbadala za kugharamia ukuta. Ameshawahi hapo awali kuzungumzia uwezekano wa kutangaza sheria ya hali ya hatari ili kukwepa masharti ya bunge.
Kikao kimeakhirishwa hadi baadae leo. Kutokana na kutofikiwa maridhiano rais Trump amelazimika kuakhirisha hotuba yake kwa taifa aliyokuwa aitoe jumanne inayokuja.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP/Reures
Mhariri:Yusuf Saumu