Mvua kubwa yatatiza shughuli Dar es Salaam
17 Desemba 2019Hali ya usafiri jijini Dar es Salaam leo imetatizwa huku shughuli kadhaa zikisimama kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia leo alfajiri. Hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara kitendo ambacho kimewakasirisha wananchi wengi hasa wakati huu ambapo miradi mingi ya miundombinu imekuwa ikiendelea kutekelezwa lakini tatizo hilo linaonekana kutotafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
Ije leo, ije kesho bado mvua itaendelea kuacha adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili linalokadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni 5, na hii leo jambo hilo limejitokeza tena wakati mvua kubwa ilipianza kunyesha kuanzia alfajiri na hatimaye kukatika nyakazi za jioni hizi.
Ingawa wakati huu Dar es salaam inaendelea kushuhudiwa upanuzi wa miundombinu kama vile barabara za kisasa zinazoendelea kujengwa pamoja na kuwepo kwa usafiri wa mwendo kasi, lakini ukweli wa mambo jiji hili bado haliko salama na mafuruko.
Barabara kadhaa ikiwemo ile ya Jangwani inayounganisha maeneo kadhaa na katikati ya jiji leo ilishindwa kuwa kuunganishi muhimu baada ya sehemu kubwa kujaa maji ambayo pia ilishuhudiwa katika maeneo mengine.
Mkazi huyo David Rwenyagira ambaye maskani yake ni eneo la Kariakoo akifanya shughuli zake huko Mbezi Beach ni moja kati ya wananchi wengi ambao hataisahau siku ya leo kutokana na adha hiyo ya mvua.
Hali inatajwa kuwa mbaya zaidi nyakati za mchana wakati kiwango cha mvua kilipoonekana kuwa cha juu. Wanachi wanaotumia usafiri wa umma kwa ajili ya kuwahi kwenye majukumu yao walilazimika kutembea umbali mkubwa kutokana na msongamano mkubwa wa magari ulioshuhudiwa katika bara bara nyingi.
Mvua hii imesababisha kilio kwa wengi ambao baadhi wanasema kwamba shughuli zao za kuosha magari na uuzaji wa reje reja wa maji zilikwama kwa leo.
Ingawa kwa wakati huu hali ya mvua imetulia kiasi lakini wengi wanawasi kama itarejea tena nyakati za usiku kwani madhara yake yakawa makubwa zaidi.