1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni awaomba radhi viongozi wenzake

18 Mei 2011

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewaomba radhi viongozi wa kigeni ambao magari yaliyowabeba yalishambuliwa kwa mawe wakati yalipokuwa yakipita katika mitaa ya mji mku wa Kampala kuhudhuria sherehe za kumuapisha.

https://p.dw.com/p/11IzG
Rais Yoweri Museveni akikakua gwaride baada ya kuapishwa tena
Rais Yoweri Museveni akikakua gwaride baada ya kuapishwa tenaPicha: AP

Siku hiyo, umati mkubwa ulikuweko uwanja wa ndege kumlaki kiongozi wa upinzani nchini humo, Kizza Besigye aliyekua akirejea nyumbani kutoka Nairobi alikokwenda kwa matibabu.

Kuwasili kwa Besigye katika siku ambayo Museveni alikuwa anaapishwa tena kuitawala Uganda, akiwa tayari ameshakaa madarakani kwa miaka 25, kulizusha machafuko katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa Kampala.

Museveni amesema gari la rais wa Nigeria lilipigwa mawe na lile la Rais wa Congo lilikaribia kufikwa na kisa kama hicho.

Amewataka radhi viongozi hao kutokana na kitendo hicho alichokiita kuwa cha kihuni na cha aibu kwa taifa la Uganda.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Mohammed Khelef