MUGABE AWASILI USWISSI:
10 Desemba 2003Matangazo
GENEVA: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili nchini Uswissi kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa Jumuiya ya Habari.Mugabe ameweza kusafiri baada ya serikali ya Uswissi kutotumia vikwazo vya kimataifa vinavyomzuia Mugabe na washirika wake kusafiri Ulaya na Marekani.Msemaji wa wizara ya kigeni ya Uswissi Alessandro Delpetre amesema serikali imeamaua kutotumia vikwazo vya kuzuia visa kwa wajumbe walioalikwa mkutanoni,ikiwa ni pamoja na rais wa Zimbabwe.Akaongezea kuwa mualiko huo umetolewa na Umoja wa Mataifa na si Uswissi.Mugabe anatazamiwa kuuhotubia mkutano huo unaoanza hii leo mjini Geneva.