Mugabe ateuliwa tena kugombania urais
14 Desemba 2007Matangazo
Chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, kimemteua rasmi rais Robert Mugabe kama mtetezi wake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2008.Uteuzi huo utamuwezesha Mugabe kuendeleza uongozi wake kwa kipindi kingine cha miaka mitano.Ameongoza nchi hiyo tangu ilipojinyakulia uhuru mwaka wa 1980.Katika hotuba yake kwa waliohudhuria mkutano wa chama mjini Harare,Mugabe amewaomba wafuasi wake kutofanya fujo dhidi ya wapinzani wakati wa uchaguzi.Mapema mwaka huu viongozi kadhaa wa upinzani walihujumiwa na vikosi vya usalama vya Mugabe.