1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mugabe anasema Zimbabwe ni yake na katu hatosalimu amri

Prema Martin/Mohamed Dahman20 Desemba 2008

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kwa mara nyingine tena amedharau mito ya viongozi wa kimataifa kumtaka ngatuke madarakani.

https://p.dw.com/p/GKIW
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.Picha: picture-alliance/ dpa

Akihutubia mkutano wa mwaka wa chama chake tawala cha ZANU-PF mjini Bindura Mugabe mwenye umri wa miaka 84 amesema Zimbabwe ni yake na kamwe hatosalimu amri.

Anasema watu pekee wenye uwezo wa kumuondowa Robert Mugabe ni wananchi wa Zimbabwe.

Hapo awali Mugabe alisema kuwa amemualika kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC Morgan Tsvangirai kwenda kuapishwa waziri mkuu katika serikali ya kugawana madaraka.Lakini Tsvangirai aliuambia mkutano wa waandishi wa habari nchini Botswana kuwa atajitoa kwenye majadiliano ya kuunda serikali yaliyokwama,ikiwa wafuasi wa MDC waliotoweka hawatoachiliwa ifikapo tarehe Mosi Januari.Alitamka hayo kufuatia kukamatwa kwa zaidi ya wanachama 42 wa MDC na wa mashirika ya kiraia.

Umoja wa Mataifa unasema,tangu mwezi wa Septemba takriban watu 1,100 wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe.Inakadiriwa kuwa zaidi ya 20,000 wengine wameambukizwa ugonjwa huo.