Mugabe afanya sherehe ya kukata na shoka kusherekea siku ya kuzaliwa
23 Februari 2008HARARE
Maelfu ya wafuasi wa rais mkongwe wa Zimbambwe Robert Mugabe wamekusanyika kusherekea siku ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo sherehe ambayo imegharimu dolla za zimbabwe Trillioni tatu ambacho ni sawa na kiasi cha dolla za Marekani milioni 1.2. Katika mji wa Beitbridge ulioko eneo la kusini la Mpakani inaarifiwa kuna shangwe na nderemo za kusherekea mwaka wa 84 tangu kuzaliwa kwa Mugabe.Kiongozi huyo anazindua kampeini yake ya kurudi tena madarakani kwa awamu ya sita.Mugabe anatumia nafasi hiyo kuwashawishi wazimbabwe waliovunjwa moyo kutokana na kusambaratika vibaya kwa uchumi wa taifa hilo wampigie Kura katika uchaguzi mkuu wa tarehe 29 mwezi ujao.Wazimbabwe kadhaa walijitokeza katika upande wa Afrika Kusini kweny eneo hilo la mpakani kupinga kiburi cha Mugabe na kutaka uchaguzi ufanyike kwa njia huru na ya Haki.Chama cha Upinzani Movement for Demkratic Change MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai pia kinazindua manifesto yake ya uchaguzi mkuu wa bunge na rais katika mji wa Mutare Mashariki ya Zimbwabwe.Inaelezwa kwamba Maelfu ya wafuasi wa Tsvangirai wanang'angania kuingia kwenye uwanja wa michezo ambao tayari umefurika maelfu ya watu.Tsvangirai ni miongoni mwa wagombea wanne watakaopambana na Rais Robert Mugabe.