1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mudavadi ajiondoa kwenye muungano wa Jubilee

Mjahid, Amina Abu Ali4 Januari 2013

Chama cha UDF nchini Kenya kinachoongozwa na Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi kimejiondoa katika muungano wa Jubilee unaojumuisha chama cha TNA cha Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na URP cha William Ruto.

https://p.dw.com/p/17DgN

Mudavadi amejiondoa katika muungano huo baada ya mkataba kati yake na Kenyatta kuvunjika ambapo Kenyatta alikuwa ameahidi kumuachia Mudavadi nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee na baadaye kumgeuka. Sasa swali ni je hatua hii ina maana gani hasa katika siasa za Kenya? Je Mudavadi aliye na nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo ana nafasi gani ya kufanikisha ndoto yake hiyo? Amina Abubakar anamuuliza maswali hayo mchambuzi wa mambo ya kisiasa nchini Kenya, Martin Oloo.