1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtuhumiwa wa ujasusi CAR aruhusiwa kurejea Ufaransa

21 Mei 2023

Mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa anayetuhumiwa kufanya ujasusi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ameruhusiwa kurejea Ufaransa kwa sababu za kiafya.

https://p.dw.com/p/4RdIP
ZAR Bürgerkrieg und Wahlen
Picha: Nacer Talel /AA/picture alliance

Licha ya kuruhusiwa kuondoka, familia ya raia huyo wa Ufaransa Juan Remy Quignolot mwenye miaka 57, imesema mapema leo kuwa bado anakabiliwa na kesi.Quignolot alikuwa gerezani kwa miezi 16, baada ya kukamatwa Mei, 2021 kabla ya kuachiliwa kwa dhamana mwezi Sebtemba. Picha zilizovuja baada ya kukamatwa kwake zilisambaa katika vyombo vya habari zilidaiwa kumuonesha akiwa na silaha lukuki zilizokamatwa nyumbani kwake mjini Bangui.Ufaransa ililaani kukamatwa kwa mwanajeshi wake huyo wa zamani katika Jamhuri ya Afrika ya kati ambayo iliwahi kuwa kuwa koloni lake. Uhusiano wa Ufaransa na nchi hiyo umezorota tangu mwaka 2018 wakati ushawishi wa Urusi ukiendelea kukua katika taifa hilo lisilo thabiti.