1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtuhumiwa wa shambulio la Berlin ni raia wa Pakistan

Oumilkheir Hamidou
20 Desemba 2016

Polisi nchini Ujerumani inasema kuna uwezekano shambulio lilikuwa la kigaidi baada ya lori kupita kwa kasi katika umati wa watu katika soko la X-Mas mjini Berlin jana usiku. Watu 12 wameuwawa na 48 kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/2UaNT
Deutschland Anschlag mit LKW auf Weihnachtsmarkt in Berlin
Picha: Reuters/F. Bensch

Kijana wa miaka 23 amekamatwa akituhumiwa kuhusika na shambulio dhidi ya soko la X-Mas mjini Berlin. Polisi wanasema tukio hilo limefanywa makusudi. Wanasema walikuwa wakimjua mtuhumiwa kwa makosa madogo madogo. Anatajwa kuwa mkimbizi wa kutoka Pakistan aliyekuwa akiishi katika kambi ya wakimbizi ya Tempelhof mjini Berlin. Gazeti la Bild linamtaja kijana huyo kuwa ni Naved B. Anasemekana ameingia Ujerumani kama mwaka mmoja uliopita.

"Wachunguzi wanaamini lori limelengwa makusudi dhidi ya umati wa watu waliokuwa wakitembea katika soko la X-Mas" amesema afisa mmoja wa polisi mjini Berlin. Ameongeza kusema wanachunguza uwezekano kama shambulio hilo ni la kigaidi.

  wiri wa mambo ya ndani Thomas de Maizière alisema "kuna mengi yanayoonyesha kuwa ni "shambulio la kigaidi. "Sababau hasa hatuzijui kwa uhakika. Hatutopumua si mpaka kila kitu kinafafanuliwa. Nisingetaka kuzungumzia neno shambulio kwa sasa ingawa kila kitu kinaashiria hivyo." Amesema waziri wa mambo ya ndani Thom,as de Maizière.

Wizara ya mambo ya ndani ya serikali kuu ya Ujerumani imeamuru bendera zishushwe nusu mlingoti  katika majengo yote ya serikali,na taasisi zote nyengine kote nchini.

Mauwa yanawekwa katika uwanja wa Breitscheidplatz shambulio lililokotokea
Mauwa yanawekwa katika uwanja wa Breitscheidplatz shambulio lililokotokeaPicha: DW/F. Hofmann

Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa mambo ya ndani wa serikali za majimbo Klaus Bouillon anazungumzia kuhusu "hali ya vita kufuatia shambulio la Berlin.

Kansela Angela Merkel anapanga kuhutubia taifa wakati wowote kutoka sasa.

Wakati huo huo viongozi wa makanisa na wawakilishi wa dini zote nchini Ujerumani wanapanga kusimamia ibada maalum kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Berlin.

Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/dpa/Reuters/AFP/KNA

Mhariri: Iddi Ssessanga