1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fulgence Kayishema afikishwa mahakamani Afrika Kusini

26 Mei 2023

Fulgence Kayishema, ambaye ni mmoja ya watuhumiwa wa mwisho wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda kupatikana, amefikishwa mahakamani mjini Cape Town siku mbili baada ya kukamatwa baada ya miaka 22 ya kutafutwa

https://p.dw.com/p/4RryH
Fulgence Kayishema
Picha: UN IRMCT

Kayishema anatuhumiwa kushiriki katika moja ya mauaji mabaya kabisa, yaliyofanywa katika kanisa la Katoliki nchini humo, ambako maelfu ya wanaume, wanawake na watoto walikuwa wamejificha.

Mtuhumiwa wa mauaji wa kimbari ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Mtuhumiwa huyo mwenye miaka 62 alionekana mtulivu wakati mwendesha mashitaka wa serikali alipokuwa akisoma mashitaka dhidi yake na baadaye hakimu Ronel Oliver aliamuru kurejeshwa kizuizini na kesi yake itasomwa tena  Juni 2. 

Afisa huyo wa zamani wa polisi aliyekuwa akisakwa kote barani Afrika, alikamatwa juzi Jumatano katika mji wa Paarl, kaskazini mwa Cape Town alikokuwa amejificha.