Mtu aliyemshambulia mume wa Nancy Pelosi afungwa miaka 30
18 Mei 2024Matangazo
Tukio hilo lilifanyika mnamo mwezi Oktoba mwaka 2022. David DePape aliyemshambulia mume wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelocy alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye nyumba ya wanandoa hao mjini San Francisco na kumshambulia Paul Pelosikatika shambulio la kutisha lililonaswa na kamera za usalama.
Awali, waendesha mashtaka walikuwa wameiomba mahakama ya shirikisho huko San Francisco kumhukumu DePape kifungo cha miaka 40 jela. Watu wengine ambao mshtakiwa huyo alikiri kutaka kuwashambulia ni pamoja na Gavana wa California Gavin Newsom, mtoto wa Rais Joe Biden, Hunter Biden, na mwigizaji Tom Hanks.