1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mtoto wa rais wa Indonesia kuwa mgombea mwenza wa urais

22 Oktoba 2023

Waziri wa ulinzi wa Indonesia na mgombea wa urais, Prabowo Subianto, amemtangaza mtoto wa kiume wa rais anayeondoka madarakani, Joko Widodo, kama mgombea wake mwenza katika uchaguzi wa mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4XsOP
Waziri wa Ulinzi na mgombea urais wa Indonesia, Prabowo Subianto.
Waziri wa Ulinzi na mgombea urais wa Indonesia, Prabowo Subianto.Picha: Alexis Sciard/IP3press/IMAGO

Hatua ya kumchagua Gibran Rakabuming Raka, aliye na miaka 36, inaweza kumpa nguvu Prabowo katika kampeni yake kufuatia umaarufu wa baba yake, licha ya  hasira za umma juu ya uamuzi wa mahakama kubadilisha vigezo vya awali vya kugombea uchaguzi ambavyo vingemzuia Gibran kugombea katika uchaguzi huo. 

Indonesia itafanya uchaguzi mkuu wa rais na bunge Februari 14.

Watu milioni 205 nchini humo kati ya raia wote milioni 270 wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo. 

Soma zaidi: Widodo achaguliwa tena rais wa Indonesia

Wiki iliyopita, Rais Joko Widodo alisema hausiki na wagombea wa urais, lakini wajuzi wa siasa za ndani wanasema rais huyo anayemaliza muda wake anataka kuendeleza ushawishi wake katika siasa za taifa hilo.

Widodo amekuwa akimuunga mkono kwa siri mpinzani wake wa zamani, Prabowo, licha ya kuonekana hapo awali akimuunga mkono Ganjar kama mgombea wa chama chake cha PDI-P