1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtoto wa Ali Bongo afunguliwa mashitaka ya uhaini

20 Septemba 2023

Mtoto wa aliyekuwa rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba pamoja na baadhi ya washirika wake wamefunguliwa mashitaka ya uhaini wa hali ya juu na ufisadi na kusekwa kizuizini.

https://p.dw.com/p/4WaWJ
Rais aliyepinduliwa madarakani wa Gabon Ali Bongo Ondimba
Rais aliyepinduliwa madarakani wa Gabon Ali Bongo Ondimba Picha: Julien de Rosa/AFP

Mwendesha mashitaka Andre-Patrick Roponat ameliambia shirika la habari la AFP kwamba walioshitakiwa ni Noureddin Bongo Valentin, mtoto mkubwa wa kiume wa Bongo, msemaji wa zamani wa ofisi ya rais Ella Ekogha, na washitakiwa wengine wanne waliokuwa na mahusiano ya karibu na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani.

Bongo mwenye miaka 64 aliyelitawala taifa hilo lenye utajiri wa mafuta tangu mwaka 2009 aliondolewa baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30, muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.