Mto Logone wavunja rikodi ya miaka 30 kwa kufurika
10 Oktoba 2024Matangazo
Taarifa ya serikali imesema kwamba kufikia asubuhi ya jana, Jumatano, maji ya mto huo yalishafikia ukubwa wa mita 8.18, kiwango ambacho hakijafikiwa kwa miongo mitatu sasa.
Soma zaidi: Chad yatoa tahadhari ya mafuriko mabaya zaidi
Waziri Mkuu Allah Maye Halina amekutana na kamati ya usimamizi wa mafuriko kukubaliana juu ya mpango wa kukabiliana na janga hilo la kimaumbile, ambalo limezikumba wilaya nane kati ya kumi za mji mkuu, N'Djamena, na majimbo 17 kati ya 23 ya Chad.
Ofisi ya Uratibu wa Huduma za Kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa inasema raia milioni 1.9 wa Chad wameathirika na mafuriko hayo.