WikiLeaks Informationsaustausch
7 Desemba 2010Mtandao wake huo umeibuka kwa kutoa taarifa nyeti za Marekani na kuutikisa ulimwengu wote.
Baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001, serikali kote duniani ziliangazia zaidi katika kubadilishana taarifa ikiwa ni mkakati wa kupambana na ugaidi.
Hata hivyo kufuatia kutolewa kwa taarifa hizo na mtandao wa WikiLeaks, sasa hali huenda ikabadilika na msisitizo ukawa jinsi ya kulinda siri.
Hatua hiyo ya kubadilishana taarifa ilikuwa muhimu sana kuliko hatari ya kutumika vibaya kwa taarifa hizo.Kutokana na umuhimu huo, kulilazimika kufanyika mabadiliko kwa idara za kijasusi na sheria nchini Marekani halikadhalika katika nchi nyingi duniani.
Balozi wa zamani Marekani katika makao makuu ya NATO Kurt Volker ambaye hivi sasa ni Mkuregenzi Mtendaji katika taasisi ya uhusiano wa Marekani na Ulaya kwenye Chuo Kikuu cha Johns Hopkins aliiambia Deutsche Welle kuwa hivi sasa kutakuwa na upinzani dhidi ya kubadilisha taarifa.
Tayari serikali kadhaa zimekwishatangaza kuwa zitadurusu na kuidhinisha jinsi gani zinakusanya taarifa, jinsi zinavyoweza kushirikiana katika taarifa hizo na kuzihifadhi taarifa muhimu.
Marekani kwa mfano hatua ina maana kuwa idadi ya watu ambao watakuwa na nafasi ya kujua taarifa hizo, itapunguzwa.
Kurt Volker anaogeza kuwa, hivi sasa maafisa katika duru za kimataifa, viongozi wa kisiasa na kibiashara, itawalazimu kuwa makini kujizuia kutoa taarifa kwa wenzao wa Marekani, na kusema kuwa hali hiyo itaathiri diplomasia ya Marekani.
Hata hivyo kwa mujibu wa Kult Volker, hatua za kubana utoaji wa taarifa zinakabiliwa na changamoto kubwa, ambayo iwapo serikali zitaamua kutotumia mtandao na kurejea katika mfumo wa zamani wa karatasi na mazungumzo ya ana kwa ana, basi kasi ya ufanisi itapungua, kuliko hivi sasa.
Mwandishi:: Michael Knigge/Aboubakary Liongo
Editor: Rob Mudge / Tamas Szabo/Mohamed Abdulrahman