1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtafaruku na wizi mjini Port-Au-Prince

28 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFg5
PORT-AU-PRINCE: Hali imezidi kokorofeka katika mji mkuu wa Haiti. Wafuasi wa Rais Jean Bertrand Aristide wameweka vizuizi na kuvitia moto katikati ya mji mkuu, kuvunja maduka na maghala ya bidhaa na kuishambulia hospitali pekee iliyobakia mjini humo. Nao umeme umekatika kabisa katika mji mkuu huo. Upande wao, waasi wanaendelea kuukaribia Port-Au-Prince na wametangaza watauzingira. - Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan ameyaita makundi hasimu ya Haiti yamalize mashambuliano yao na kuusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa kwa njia za amani. Hali imezidi kudhoofika nchini humo, ilisisitiza taarifa ya Bwana Annan kutoka makao makuu ya UM mjini New York. Kwa mara nyingine Rais Aristide amekataa kujiuzulu kabla ya kumalizika muda wa utawala wake hapo 2006. Nayo Marekani inazingatia kupeleka manuwari zake tatu katika mwambao wa Haiti.