1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

UN: Haiti inahitaji walinda amani 5,000 kurejesha utulivu

29 Machi 2024

Mtaalam wa masuala ya Haki na Migogoro wa Umoja wa Mataifa anaefuatilia mzozo nchini Haiti, amesema nchi hiyo inahitaji kati ya maafisa walinda amani 4,000 na 5,000 ili kukabiliana na ghasia za magenge ya wahalifu.

https://p.dw.com/p/4eF3H
Uhalifu katika Mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince
Askari wa Haiti wakiwa kwenye doria katika mji mkuu Port-au-Prince ambao unakumbwa na ghasia za magenge ya wahalifuPicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Mwaka jana, William O'Neill alikadiria kuwa Haiti ilikuwa ikihitaji kati ya askari 1,000 na 2,000 ili kukabiliana na magenge ambayo kwa sasa yamejiimarisha na kuendesha mashambulizi dhidi ya raia, hospitali, shule, benki, uwanja wa ndege na taasisi nyingine muhimu.

O´Neill amesema idadi hiyo imeongezeka kwa kuwa  kwa sasa hali ni mbaya mno nchini Haiti na kwamba askari hao wa Umoja wa Mataifa wanahitajika ili kuwasaidia Polisi wa Haiti kurejesha udhibiti wa usalama na kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu.