Msukosuko wa fedha duniani
25 Septemba 2008Kwa muujibu wa waziri wa fedha wa Ujerumani Bw.Peer Steinbruck, athari zinazotokana na msukosuko wa soko la fedha la Marekani, bado hazionekani.Kinachodhihirika kwake, ni kuwa msukosuko huu, utaathiri ukuaji wa uchumi kote ulimwenguni na kuongoza katika ukosefu wa kazi.
Kwa muujibu wa waziri huyo,tujifunze darasa linalotokana na hali iliozuka na hatua zichukuliwe kuzuwia balaa kama hili lisizuke tena.Kwa mfano, Bw.Steinbruck alipendekeza mabenki yadhibitiwe barabara shughuli zao.
Mfumo wa fedha ulimwenguni umepatwa sasa na msukosuko mkubwa kabisa tangu ule wa ile ilioitwa "ijumaa nyeusi" 1929.Msukosuko huu kama iliopita,umesababishwa na wanadamu wenyewe. Chanzo chake ni makosa,dharau ,uzembe, kufurutu ada na zaidi kabisa, ni uchu wa faida nono.Uroho ulikuwa hata mkubwa zaidi kuliko fahamu.
Na hii ndio mbaya sana.Lakini mbaya hata zaidi ,ni kuwa masoko ya fedha yakiishi ulimwengu wake binafsi- nje kabisa na sayari yetu na yalikwepa kabisa kudhibitiwa na vyombo vya dola.
Kuna wachache waliofaulu mnamo miaka iliopita kujitajirisha mno ,lakini sasa ambapo ulimwengu wa fedha umeporomoka chini,sote tunabidi kulipa gharama zake.Serikali hazina njia nyengine isipokuwa kutumia fedha za walipa kodi ili kuuokoa mfumo wa kibepari kuanguka kabisa.Wakati huo huo serikali hizo zina jukumu la kujifunza darasa kutoka msukosuko huu.Ikiwa si hivyo, hatua hizi za sasa za ukokozi zinashikamana na hatari za kuripua balaa jengine siku za mbele.
Ni kwa kuuchungua tu ugonjwa ndipo unapoweza kuupatia dawa yake mujarabu.Uchunguzi wa ugonjwa uliozuka unabainisha kuwa maradhi yameatuwama hasa Marekani. kutokana na msukosuko huu,Marekani itapoteza mamlaka yake ya kuwa dola kuu kifedha duniani.Kwani, wakati Marekani,serikali,viwanda vyake na makampuni,watu majumbani wamekalia mlima wa madeni, nchi nyengine zinasimamia vitita vikubwa vya fedha.Na hasa China,dola zinazozalisha mafuta na hata Urusi. Marekani ndio wakopeshaji wakubwa ulimwenguni.Lakini sasa kutegemeana kifedha ni kwa kila mmoja inamtegemea mwenzake kinyume na hapo kabla.Kuporomoka kwa mfumo wa fedha wa Marekani kutaichukua dunia nzima shimoni.
Na hii lazima izuwiliwe isitokee.Kwanza katika kuonesha umoja na mshikamano na Marekani ,kwanza kila nchi itatue matatizo yake.Halafu kwa pamoja ni kujaribu kuzuwia athari zisizuke na kuchukua hatua kuimarisha mfumo wa fedha ulimwenguni.
Katika kufanya hivyo, ndipo shauri la waziri wa fedha wa Ujerumani Peer steinbruck yafaa kutiwa maanani.Ameitisha kwa msaada wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) kuyawekea masoko yote ya fedha kanuni kali za kufuata.Miongoni mwa kanuni hizo shughuli za kibanki ziwekwe wazi zionekane na mabenki yajitwike jukumu la kuwa na uwezo mkubwa wa akiba za fedha .Mameneja wa mabanki watwikwe dhamana zaidi kuliko ilivyo sasa kwa makosa yatakayofanyika na pakomeshwe mtindo wa mabanki wa kusaka faida nono kupita kiasi.
Shabaha hapa ni kuzuwia hatari zaidi kutokea kwa masoko ya fedha.Kwani hatari hizo zikiwa haziwezi tena kudhibitiwa, basi zaweza zikautosa uchumi mzima wa dunia kwenye balaa.tayari sasa msukosuko huu wa fedha unaathiri ukuaji wa uchumi kabla wakati .Kwani hata Ujerumani ikijikuta ikistawi tena kiuchumi na sasa...?