MSIMU MPYA WA VIKOMBE VYA KLABU BINGWA ZA AFRIKA UMEANZA.FINALI YA KOMBE LA VIJANA COTONOU NA KASHFA KATIKA DIMBA LA UJERUMANI.
27 Januari 2005-SHIRIKISHO LA DIMBA LA UJERUMANI DFB NA KASHFA YA RIFU MCHEZA KAMARI
-MSIMU MPYA WA VIKOMBE VYA KLABU ZA AFRIKA
NA FINALI LEO YA KOMBE LA VIJANA LA AFRIKA MJINI COTONOU.
Shirikisho la dimba la Ujerumani (DFB) limetangaza kati ya wiki hii kwamba limemfungulia mashtaka rifu Robert Hoyzer,ambae anatuhumiwa pengine akicheza kamari juu ya matokeo ya mechi yeye akichezesha uwanjani.Limepeleka mashtaka kwa mshtaki mkuu wa serikali.
DFB limesema juu ya hivyo ,litasonga mbele na uchunguzi wake binafsi juu ya mkasa huu kuhusu mechi kadhaa zilizochezeshwa na rifu huyu.
DFB inataka hasa kufumbua kitandawili nani akicheza kamari kwa vitita vikubwa juu ya mechi zilizochezeshwa na rifu Robert Hoyzer na iwapo kuna mahusiano yoyote kati ya wacheza hao kamari na rifu Robert Hoyzer.
Kuhusu kisa cha rifu Hoyzer, waziri wa ndani wa Ujerumani anaehusika pia na michezo Otto Schily amedai uchunguzi barabara ufanywe juu ya tuhuma hizi za kupanga matokeo ya mechi.Inakisiwa hadi mechi 5 zilipita namna hiyo.
Mkurugenzi wa Shirikisho la dimba la Ujerumani ,Theo Zwanziger alifichua mwanzoni mwa wiki kuwa rifu Robert Hoyzer alipangilia matokeo ya hadi mechi 5 kwa ajili ya kuvuna fedha katika mchezo wa kamari .
Rifu Hoyzer alianza kuchunguzwa baada ya timu ya SC Paderborn isiocheza katika Ligi na timu ya daraja ya tatu kuthubutu kuishinda timu ya Hamburg ya daraja ya kwanza hapo August 21, mwaka jana.Katika mpambano huo alitoa mikwaju 2 ya adhabu ya penalty kwa Paderborn na kumtimua mshambulizi wa Hamburg nje ya uwanja Emile Mpenza kwa kuwa tu alinungunika.Paderborn ilitoka nyuma 2:0 na mwishoe ilishinda kwa mabao 4-2.
Hii ni kashfa kubwa ya dimba nchini Ujerumani tangu kupita zaidi ya miaka 30.Ilifichuliwa na marifu 4 waliodfai wamefanya hivyo kuepusha dhara katika dimba la Ujerumani.Rifu Zoyer amejiuzulu kama rifu.
Wakili wa rifu Robert Hoyzer aliliambia gazeti moja kuwa kile shirikisho la dimba la Ujerumani DFB lilichofanya ijumaa ya wiki iliopita ni kumtiakitanzi kabisa mteja wake.
Ujerumani ilikumbwa na kashfa kubwa katika dimba 1971 na wachezaji jumla ya 53 waliadhibiwa kwa vikwazo.Makocha 2 walihusika pia pamoja na wakuu sita wa klabu pamoja na timu za Armenia Bielefeld na Kickers Offenbach.
VIKOMBE VYA KLABU BINGWA ZA AFRIKA:
Firimbi ililia jana kuanzisha na mpema msimu wa mwaka huu wa vikombe vya Afrika.Kinyan’ganyiro cha Champions League-Kombe la klabu bingwa barani Afrika.
Mshindi wa taji hapo Novemba mwaka huu, ndie ataeiwakilisha Afrika huko Japan desemba mwaka huu katika Kombe la dunia la klabu bingwa za mabara 5.
Zanzibar imekaribishwa kwa mara ya kwanza katika kinyan’ganyiro cha mwaka huu cha vikombe vya Afrika.Ikishiriki katika changamoto 2:Katika Kombe la klabu bingwa Zanzibar inawakilishwa na KMKM ambayo jioni hii imekuwa uwanjani Nairobi kupambana na Tusker Fc ya Kenya.
Kwa upande mwengine, Kampala City Council ya Uganda inazuru visiwani ,kwani huko ina miadi na Kipanga huko zanzibar kwa changamoto ya Kombe la shirikisho la dimba (CAF).
Changamoto za Kombe la klabu bingwa barani Afrika zinacheza kwanza mapambano 3 ya kutoana kabla klabu 8 za mwisho kuumana katika mfumo wa Ligi kuanzia Juni.
Leo ni finali ya Kombe la vijana la Afrika mjini Cotonou,Benin.Katika changamoto za kati ya wiki za nusu-finali , Nigeria iliondoka suluhu uwanjani na Morocco kwa kuagana kwa mabao 2:2.
Benin ilizabwa mabao 4:1 na Misri.Timu ya Benin ya chipukizi chini ya umri wa miaka 20 iliongoza kwa bao alilotia Maiga Gariga Abou dakika ya pili tu ya mchezo, lakini jibu la Misri lilikuja dakika ya 83 ya mchezo pale Farag aliposawazisha.Baadae changamoto ya mikwaju ya penalty ikaamua hatima ya Benin nyumbani
Misri ilishinda zahama hiyo kwa mabao 4:1 na kuitoa Benin.Timu zote mbili ziliovaa utambi mweusi mkoni na zilinyamaa kimya dakika moja kuomboleza kifo cha kipa wa Benin Samiou Yessoufou,alieuliwa akiwa na umri wa miaka 18 hapo Januari 16.Katika nusu-finali ya pili,Nigeria ilichapa Morocco mabao 5-3 pia katika changamoto ya mikwaju ya penalty kufuatia kutoka suluhu mabao 2:2.
Ama kuhusu kifo cha kipa Yousoufou,
Polisi ya Benin imewatia nguvuni watu 6 kwa mashtaka ya mauaji ya kipa wa Benin, alieuliwa siku 1 baada ya Bein kuzabwa mabao 3-0 na Nigeria katika dimba la ufunguzi.Polisi inamska mtu 7.
Awali wakuu wa dimba walisema kipa Yessoufou alipigwa na mashabiki waliokasirika kwa kuachia mabao hayo.Polisi lakini wanadai kipa huyo ameuliwa wakati wevi wakajaribu kuiba simu yake ya mkono-handy.
Mbabe wa zamani wa wezani wa juu ulimwenguni, Lary Holmes amesema ingawa amenenepa mno na ana umri wa miaka 55,hatahivyo ana hamu ya kuingia ringini kupambana na bingwa wa zamani mzee George Foreman mwenye umri wa miaka 56.larry Holmes ameeleza kwamba azma yake sio kurejea tena ringini kama zamani,la,hasha.hamu yake tu ni kutwangana na George Foreman.
.