You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Msichana Jasiri
Kila msichana ana nafasi sawa kuwa jasiri - Msichana Jasiri!
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Wasichana wanaodhamiria kuwa wanamitindo mahiri
Kutana na wasichana wanaopigania ndoto zao licha ya kuwa wanatoka katika mazingira duni lakini hali hiyo haijawa kisiki kwao. Azma yao kuu ni kutaka kuyafikia malengo yao ili wawe wanamitindo mahiri. Mtangazaji chipukizi Hadija Halifa anasimulia zaidi kwenye video zetu za Msichana Jasiri.
Mchoraji wa picha za kufikirika
Anatumia sanaa ya uchoraji wa kufikirika ili kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya sanaa na ili sanaa ya uchoraji ifike mbali zaidi na kutambuliwa na wengi. Lakini je nafasi ya wazazi katika kuamini vipawa vya watoto wao iko wapi? Na wanatoa nafasi gani katika kuvikuza na kuviendeleza vipaji hivyo? Mtangayaji chipukizi Hadija Halifa na mengi yaidi kwenye video hii ya Msichana Jasiri.
Msichana mwenye kipaji cha sanaa ya sarakasi
Mischana mdogo anaefanya sanaa ya sarakasi na kutumia mitandao ya kijamii kujinadi kwa manufaa ya kufikia malengo yake licha ya kuwa na umri mdogo lakini anaweza kubadili kifra za wasichana wengi na kuweza kufikia malengo yao
Msichana Jasiri: Fasihi andishi mitandaoni
Getrude Mligo ni binti ambaye ameona ombwe katika mitandao ya kijamii na akaamua kutumia fasihi andishi ili kuelimisha wasichana kutumia mitandao ya kijami kwa njia yenye manufaa. Ungana na Hadija Halifa ambaye amepiga stori na Getrude.#msichanajasiri
Farhat Sheikh wa 20 Bob Movement ya Kenya
Kutana na msichana jasiri Farhat Sheikh anaesaidia jamii katika maeneo yanayomzunguka kupitia asasi iitwayo 20 Bob Movement ya Kenya. Zaidi ungana na Fathiya Omar.
Kutumia vijiti vya lambalamba kama malighafi mujarabu kusanifu mapambo
Anatumia vijiti vya lambalamba kutengeneza mapambo ya ofisini na majumbani. Alichukua hatua hiyo baada ya kukosa mkopo wa chuo kikuu hivyo ilimlazimu kutengeneza bidhaa ili aweze kujikimu. Wakati huu akisubiri kupata ajira anauza mapambo alotengeneza kupitia mtandao wa Instagram. Mwanahabari chipukizi Hadija Halifa anasimulia mengi zaidi kuhusu Msichana huyu Jasiri Saida Kaasim.
Getrude Clements, mwanaharakati wa afya ya uzazi Tanzania
Matunda ya safari yake yalianza kuonekana mwaka 2016 alipowawakilisha vijana na watoto wote ulimwenguni katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu athari za kimazingira. Baadae ombwe lililopo la elimu ya afya ya uzazi ndilo linalomsukuma kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha umma, na anashuhudia matokeo mazuri. Mwanahabari chipukizi Hadija Halifa na mengi zaidi kwenye #Msichana Jasiri
Msichana Jasiri: Naibu Spika-Bunge la Vijana EAC
Katika umri mdogo amefaulu kufanya mengi kumwakilisha msichana katika bunge la vijana la Afrika Mashariki kadhalika katika masuala ya uandishi wa habari za kijamii. Hadija Halifa amezungumza na Khayyam Mustapha ambaye leo ndio msichana wetu jasiri. #msichanajasiri
Mafunda Faki, balozi wa vijana Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki
Licha ya utamaduni wa jamii inayomzunguka, Mafunda Faki ambaye ni msichana anayeiwakilisha Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki amepiga hatua na kuwa mfano kwa vijana wenzake. Ushauri na ushawishi wake kwa vijana wenzake ni upi? Je ana malengo yapi? Mwanahabari Chipukizi Hadija Halifa anamuangazia kwenye #MsichanaJasiri.
Ines Raquel, mwanamuziki chipukizi kutoka Burundi
Sauti yake ni ya kutoa nyoka pangoni. Kipaji chake cha uimbaji pia kinawavutia wengi. Katika makala Msichana Jasiri tunamuangazia msanii huyu Ines Raquel ambaye sauti yake imeshaanza kuyateka masikio ya wapenzi wengi wa muziki.
Uwanasoka bora bila kusaliti utamaduni
Baadhi ya wazazi wamekuwa wakipinga watoto wao wa kike kuingia katika mchezo wa soka kwa hoja kwamba ni kinyume na utamaduni, licha ya kuwa baadhi yao wana ndoto ya kuwa wanasoka bora Afrika. Fuatilia video hii ya Msichana Jasiri, ambapo mwanahabari chipukizi Hadija Halifa anazungumza na wasichana wa Zanzibar.
Ruth Naam msusi mdogo anaeonesha njia
Kutoka utaalamu wa masoko hadi katika stadi za ususi. Baada ya kusaka namna ya kuajiriwa aliamua kujifunza kusuka ambapo sasa anatumia taaluma yake ya darasani kwa kusaka wateja ili kujipatia kipato. Ruth Naaman ndiye jasiri wetu wa leo.
Happy Sanga shujaa wa ukombozi wa wanafunzi
Happy Sanga, msichana kiongozi aliyeacha alama katika nyanja ya elimu Tanzania, zaidi mtazame katika vidio ya msichana jasiri,
Fahamu siri za Jessica, mjasiriamali kijana
Ndoto yake ni kuona vijana wengi wanafanikiwa, hilo linamfanya anakuwa katika harakati nyingi kwa kutumia majukwaa ya elimu, siasa na hata Sanaa kufikisha dhima yake kwa jamii na hili linamfanya @jessicamshama kutunukiwa tuzo zaidi ya kumi kutambua mchango wake. @miss_hadijahalifa anazungumza naye.
Msichana Jasiri Betina Contine - Utamaduni ni wetu Watoto ni wetu
Isikilize makala ya Msichana Jasiri leo hii iliyoandaliwa na Salma Mkalibala ambapo amemuangazia msichana Betina Contine.
Msichana Jasiri: Fahamu sanaa ya 'Uoni'
Kundi la wasichana la jasiri linafanya sanaa ya uoni. Hii ni sanaa ya kufikirika kwa kutumia picha halisia na zile za kubuni na rangi. Kundi hili linatumia sanaa hiyo ngumu kufikisha changamoto zilizo kwenye jamii yao. Mwanahabari Chipukizi Hadija Halifa amewatembelea katika sehemu yao ya kuandaa kazi zao jijini Dar es Salaam. Tizama zaidi kwenye Msichana Jasiri
Latifa Mohammed mwanaharakati wasichana
Ameona kuna haja ya kutoa muda wakekulifikia kundi la wanawake kuwawezesha kielimu na mawazo ili kuwakomboa kiuchumi kupitia taasisi yake. Msichana jasiri wiki hii ni Latifa Mohammed ambaye amezungumza na Hadija Halifa @miss_hadijahalifa.
Khadija Mwanamboka, mbunifu awajengeaye wasichana kujiamini
Khadija Mwanamboka ameamuwa kutumia jukwaa lake la Ujuzi Fashion Hub kuwasaidia wasichana kufikia malengo yao.
Diana Saria: Binti anayehamasisha mabinti kuacha biashara ya ngono
Biashara haramu ya ngono katika jiji la Arusha imekuwa ikiendelea katika eneo hilo la kaskazini mwa Tanzania. Japo kumekuwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa za kukomesha biashara hii, imeendelea kushamiri hasa katika miji mikubwa.
Meena Ally anayetumia habari kusaidia vijana
Akiwa na umri mdogo, tayari Meena Ally ameshajizolea umaarufu kutokana na utangazaji wake mahiri wa vipindi vya vijana.
Ufugaji wa Panya kwa matumizi ya kisayansi
Ni katika umri wa miaka 18 tu, wasichana hawa wameona changamoto ya uhaba wa panya kwa ajili ya matumizi ya kisayansi nchini Tanzania na kuchangamkia fursa. Sasa kwa namna gani wameanza ufugaji? #MsichanaJasiri 23.04.2021
Msichana mwenye ndoto ya kuwa mwandishi habari
Katika jamii nyingi mtu anapokuwa na mapungufu ya kimaumbile ni nadra kuwa na maisha sawa na wengine, hii ni kutokana na unyanyapaa wanaokabiliana nao, katika video ya msichana jasiri leo@miss_hadijahalifa anazungumza na msichana mwenyendoto ya kuwa nyota katika taaluma ya uandishi. Je anapowa ushirikiano na jamii yake?
Msichana Jasiri- Sarakasi
Sanaa ya sarakasi ilionekana kufanywa na wavulana zaidi, sasa mambo yamebadilika wasichana nao wananchangamkia fursa hiyo adhimu na ya kuburudisha. Hadija Halifa ni nahodha wako.
Msichana Jasiri: Hadija Halifa atuzwa
Mtangazaji wetu chipukizi wa kipindi cha #MsichanaJasiri hapa DW Kiswahili Hadija Halifa, atuzwa kama 'Super Woman' kutokana na juhudi zake za kuhamasisha wasichana. Amepata tuzo hiyo siku hii ambayo pia ni ya kimataifa ya wanawake. Je ungependa kumwambia Hadija chochote?
Msichana Jasiri: Msichana mchuuzi wa maji Dar Es Salaam
Mtaji wa shilingi 2600 imemuongezea thamani ya upambanaji Katika biashara yake ya kuuza maji Katika foleni za jiji kuu la kibiashara Tanzania. Je wewe unaeza kufanyia nini shilingi 2600 za Tanzania, endapo uko nchini humo? Tazama video hii ya Msichana Jasiri, mtangazaji chipukizi Hadija Halifa akujuze zaidi
Mapambano dhidi ya mila ya ukeketaji
Msichana Jasiri hii leo unakupeleka hadi huko Umasaini nchini Tanzania, ambako bado mila ya ukeketaji inaendelezwa. Na hii leo kipindi hiki kitaangazia kwa kina harakati za kukabiliana na mila hiyo inayopigwa vita kote ulimwenguni. Ni harakati gani hizi? Ungana na Veronica Natalis.
Ismat ni mwanasarakasi jasiri licha ya ulemavu
Mohammad Ismat (29) kutoka Mombasa, Kenya ni mchezaji densi, mwana sarakasi na pia mwalimu wa Yoga. Kijana huyu ameweza kufanya yote hayo licha ya kuwa na ulemavu wa macho alioupata baada ya kupata saratani. #Kurunzi
Angel Nyigu msichana aliyepata mafanikio kwenye Dansi
Kutana na Angel Nyigu msichana jasiri aliyepata mafanikio kwenye unenguaji.
Watoto wanaharakati wa sheria za barabarani Tanzania
Kutana na wanahabari watoto nchini Tanzania wanaoendeleza kampeni za usalama barabarani kupitia vipindi vya redio. Mwandishi wa habari chipukizi Hadija halifa anawaangazia pamoja na juhudi zao kwenye makala ya Msichana Jasiri
Miriam Yohana binti mtunza familia
Licha ya maradhi ya kifafa alionayo, Miriam Yohana analo jukumu la kulea wadogo zake watatu, mama yake mwenye tatizo la Afya ya akili kutokana na babake kuwa mbali na familia kwa kipindi kirefu bila mafanikio. Khadija Khalifa amemtembelea na kuzungumza nae. #kurunzi
Simrang (16) msichana jasiri anaesimamia biashara ya mabilioni ya shilingi
Msichana wa umri wa miaka 16 anasimamia na kuongoza biashara yenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Hii ni kutokana na kuaminiwa na familia tangu angali mdogo. Je wewe katika umri wa miaka 16 umefanya nini? Hadija Halifa mtangazaji chipukizi anazungumza nae kwenye video hii ya #MsichanaJasiri.
Msichana Jasiri: Msichana anayechora picha kujikimu chuoni
Mhelepu Shilingi amewashangaza wengi baada ya kutumia muda wake wa ziada nje ya mgahawa mjini Dar Es Salaam nchini Tanzania akichora picha za watu ili kupata fedha kwa ajili ya mahitaji yake chuoni na kiasi, kwa familia yake iliyopo Morogoro. Watu wengi wamempa taji la ujasiri. Mtangazaji Chipukizi Hadija Halifa anaangazia juhudi zake.
Mariam Iddi, mmilki wa mgahawa unaouza vichwa vya kuku
Katika makala ya Msichana Jasiri, leo tunamuangazia Mariam Iddi ambaye ni mjasiriamali na mmilki wa mgahawa unaouza vichwa vya kuku, utumbo, na hata firigisi. Kitu gani kilimpa msukumo wa kuanzisha mgahawa huu ambao umekuwa kivutio kikubwa kwa wateja? Msimulizi katika video hii ni mtangazaji chipukizi Hadija Halifa.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 3 wa 3
Ukurasa unaofuatia